BY ISAYA BURUGU 22ND DEC 2022-Gibson Gathu Mbugua  aliyewahi  kuwa kiongozi wa mashtaka katika kipindi maarufu cha Vioja mahakamani kinachopeperushwa kwenye runinga yakitaifa ya KBC  ameaga dunia.

Mbugua  alikuwa amefanyiwa  upasuaji kubadilishiwa figo  katika hospitali ya Mediheal mjini Eldoret. Hata hivyo baada ya kuruhusiwa kuondoka hospitalini, alikumbwa na matatizo ya kupumua siku chache baadaye na akalazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi akiwa amepoteza fahamu.

Kwa mjibu wa mwenzake waliofanya naye kazi kwa karibu ,Mbugua anaripotiwa kupoteza fahamu kwa muda wa miezi mitatu hadi kuaga dunia kwake mapema leo.

i

December 22, 2022