Anthony Blinken

Serikali ya Marekani imetangaza hatua ya kupeleka silaha zaidi Ukraine zilizo na thamani ya Yuro milioni 725. Kulingana na taarifa kutoka katika Ikulu ya White House silaha hizo ni pamoja na mifumo ya makombora ya masafa marefu ya HIMARS, magari ya kivita na vifaa vya matibabu.

Waziri wa Mambo ya kigeni wa Marekani Antony Blinken, amesema taifa lake litaendelea kuiunga mkono Ukraine katika nia yake ya kulinda uhuru wake. Blinken amesema silaha wanazotoa zitaisaidia Ukraine kujilinda zaidi katika uwanja wa mapambano. Silaha hizo zinasemekana kutolewa katika idara ya Ulinzi hii ikiwa ni kwa mujibu wa wizara hiyo. Tangu Urusi ianze kumvamia jirani yake Ukraine tarehe 24 mwezi Februari Marekani chini ya utawala wa Joe Biden imetuma msaada wa kijeshi unaogharimu Yuro bilioni 18.3 hadi sasa. | Maelezo zaidi kwa udhamini wa DW

 

October 15, 2022