Makala ya 12 ya mashindano ya WASCO yanayohusisha kampuni za usambazaji wa maji kutoka maeneo yote ya taifa yataandaliwa katika Kaunti ya Narok mwezi Aprili 2023. Haya ni kwa mujibu wa waziri wa maji na usafi wa mazingira katika kaunti ya Narok Job Ole Kiyapi ambaye amekumbatia nafasi ya kuandaa michuano hii kwa mikono miwili, michezo  inayowahusisha zaidi ya wafanyakazi 2500 kutoka katika kampuni 40 za maji kote nchini.

Akizungumza katika uga wa Ole Ntimama mjini Narok siku ya Jumamosi 08.Oktoba 2022 katika hafla ya kupokezwa kibali cha kuandaa mashindano haya, Ole Kiyapi alisema kuwa hii ni nafasi ya kipekee kwa washikadau katika sekta ya maji kusaidiana na kuelimishana ili kuweza kuinuka. Kwa upande wake, waziri wa maji katika serikali ya Kaunti ya Kisumu ambayo ilikua mwenyeji wa awamu iliyopita Salmon Orimba ametoa changamoto kwa usimamizi wa kaunti ya Narok kuandaa hafla ya kufana na kuwezesha makala ya 12 kufana hata Zaidi, kauli yake ikiungwa mkono na Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Usambazaji wa Maji Katika kaunti ya Narok NARWASCO Bw. Stanley Kuyoni ambaye ameahidi ushirikiano wake katika kufanikisha mashindano haya.

Mashindano haya ambayo hutumiwa kama nafasi ya kampuni za usambazaji wa maji kujimarisha na kuendeleaza ujuzi wao katika utoaji wa huduma za maji kwa wananchi hususisha michezo kama vile michezo ya mpira, draught, dats, chess, scrabble, riadha, mashindano ya kwaya na hata mashindano ya ngoma za kitamaduni.

Washiriki katika makala ya 11 ya mashindano ya WASCO yaliyoandaliwa katika kaunti ya Kisumu.

 

October 8, 2022