Rais William Ruto yuko katika taifa jirani la Uganda, ambapo anatarajiwa kuwa miongoni mwa viongozi watakaohudhuria hafla ya maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru katika taifa hilo. Kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari, Rais Ruto aliondoka nchini adhuhuri ya leo na kupokelewa na rais wa Uganda Yoweri Museveni muda mfupi baadaye. Katika ziara yake, rais anatarajiwa kuandaa mazungumzo na mwenyeji wake kuhusu ushirikiano na kuimarisha uhusiano baina ya mataifa haya mawili.