By Isaya Burugu,Oct 08,2022-Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja  ameagiza kubuniwa kwa kamati  ya maswala ya uchukuzi itakayojumuisha wahusika  mbali mbali wa sekta hiyo  itakayosimamia mikakati ya kupanga mipango ya kukabili tatizo la msongamano wa magari katikati mwa jiji.

Sakaja amehoji kuwa mashirika mbali mbali yanayoshughulikia uchukuzi na udhibiti ya msongamano yamekuwa yakifanya kazi kila moja kivyake na wakati umefika kwa mashairika hayo kufanya kazi Pamoja ili kuleta mwelekeo jijini .

Amesema  kaunti zingine nne  zinazojumuisha eneo la Nairobi za Kajiado.Kiambu ,Machakos,na Muranga tayari zimebuni kamati yao ya uchukuzi.Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya NTSA George Njao aliyekuwa kwenye mkutano huo ameunga mkono hoja ya kuwa na kamati moja ya uchukuzi wa Nairobi.

 

 

October 8, 2022