Madaktari humu nchini wametangaza kusitishwa kwa mgomo uliokuwa umeratibiwa kuanza kuanza hio kesho tarehe 6 mwezi Januari. Hii ni baada ya kuafikia makubaliano katika kikao cha mazungumzo kati ya wawakilishi wa matabibu, Baraza la Magavana na Wizara ya Afya.

Katika kikao hicho kilichoandaliwa hii leo, muungano wa KMPDU pamoja na asasi hzio mbili za uongozi waliafikiana kuundwa kwa kamati katika kiwango cha Kaunti, itakayoangazia utekelezaji wa mkataba wa makubaliano wa mwaka 2021.

Katibu mkuu wa KMPDU Dr. Davji Atellah alisema kuwa hata ingawa makubaliano hayajaafikiwa ipasavyo, wameamua kukumbatia mazungumzo kwa nia ya kupata suluhu la kudumu. Aidha amesema kuwa mkataba wa maelewano wa 2021 utatekelezwa kikamilifu ili kusaidia kuimarisha kiwango cha huduma za afya kote nchini.

January 5, 2023