Mkuu wa Baraza la Mawaziri nchini Musalia Mudavadi ameongoza baraza la mawaziri pamoja na viongozi wengine, katika kikao cha kwanza cha mashauriano, kilichoandaliwa katika hoteli ya Mt. Kenya Safari Club eneo la Nanyuki katika kaunti ya Laikipia.

Kikao hicho ambacho cha siku nne, kiliitishwa na rais William Ruto ili kusaidia katika kuweka mipango kabambe ya kufanikisha ajenda yake ya maendeleo kwa wakenya. Mawaziri pamoja na washauri wa serikali pamoja na viongozi wengine akiwemo aliyekuwa jaji mkuu nchini David Maraga, walihudhuria kikao cha leo.

Katika vikao hivi, rais William Ruto na kikosi chake cha kuiendesha serikali, wanatarajiwa kuweka mipango ya jinsi ya kuthibiti gharama ya maisha pamoja na maswala mengine ya muhimu kama vile utovu wa usalama katika maeneo kadhaa ya ukanda wa bonde la ufa.

January 5, 2023