Matayarisho ya kumpokea rais William Ruto katika kaunti ya Narok hio kesho yamekamilika rasmi. Haya ni kwa mujibu wa gavana wa kaunti ya Narok patric Ole Ntutu, ambaye aliyezungumza Jumamosi mchana baada ya kuiongoza kamati ya usalama katika kaunti kufanya uchunguzi wa matayarisho haya katika uwanja wa William Ole Ntimama.

Gavana huyu alieleza kuwa mkutano wenyewe unapania kuwa wa maombi ya kurudisha shukrani kwa Mwenyezi Mungu.


Kauli ya gavana Ntutu iliungwa mkono na kamishena wa kaunti ya Narok Bw. Isaac Masinde, ambaye aliwarai wananchi kuwasili katika uga wa michezo wa William Ole Ntimama kabla ya saa mbili asubuhi ili kumsubiri kiongozi wa taifa.

Wakati huo huo, wazee wa baraza la jamii ya maa humu nchini wameeleza kwamba wako tayari kumlaki na hata kumkaribisha kiongozi huyo wa taifa.

Akiwahutubia wandishi wa habari mjini Narok, mwenyekiti wa baraza hilo humu nchini Keleina Nchoe amesema jamii ya maa inaunga mkono serikali kutekeleza ajenda zake kwa wananchi wa Narok.

Kauli yake imeungwa mkono na mwenyekiti wa baraza hilo kaunti ya Kajiado David Sankori aliyesema kuwa wazee wa baraza la jamii ya Maa wanaendelea kushabikia hali ya amani na utulivu inayoshuhudiwa nchini.

January 28, 2023