BY ISAYA BURUGU ,30TH JAN,2023-Shughuli ya kuwasajili  jumla ya wanafunzi milioni 1.2 waliofanya mtihani wa gredi ya sita KPSEA, kujiunga na  shule ya junior secondary chini ya mtaala wa CBC imengoa nanga kote nchini hivi leo.

Uchunguzi uliyofanywa na idhaa ya redio Osotua katika shule mbali mbali zilizopewa idhini kuwasajili wanafuzi hoa katika kaunti ya Narok umebaini kuwa hali ni shwari.

Wazazi walianza kufika katika shule hizo mapema asubuhi kufuatilia shughuli hiyo.Aidha hali imekuwa kama hiyo kwenye kaunti jirani ya Nakuru huku shughuli hiyo ikiendelea katika shule 1200 zilizoidhinishwa

Kuhusu swala la sare na mahabara, maafisa wanasema mikakati mwafaka imewekwa.

 

 

 

 

 

 

 

January 30, 2023