Nick Salat

Chama cha KANU kimetoa orodha ya wanachama watakaohudumu katika kamati ya kinidhamu ili kusikiliza na kutoa uamuzi wao dhidi ya aliyekuwa katibu wa Chama hicho Nick Salat ambaye alisimamishwa kazi tarehe 15.12.2022.

Kamati hiyo ya nidhamu itaongozwa na Mbunge wa Kilgoris Julius Sunkuli na itawajumuisha Wanachama wengine ambao ni Pamoja na Bi Gladwell Tungo (Makamu Mwenyekiti wa kamati), Bw Arnold Otieno (katibu), Bw Josephine Leado, Bw Ali Ogle na Bw Joshua Mukirae.

Kamati hiyo ina jukumu la kusikiliza kesi dhidi ya Salat na kutoa uamuzi wake kuhusu madai ya ukosefu wa nidhamu wakati wa kikao cha viongozi waliochaguliwa wa chama cha KANU kilichaoandaliwa tarehe 3 mwezi huu wa Disemba 2022.

Kwa upande wake, Bw. Salat hata hivyo ameeleza kuwa huenda akakosa kupata haki katika kamati hiyo, akidokeza kwamba wanakamati hao ni watu wenye uhusiano wa karibu na kinara wa chama hicho Gideon Moi.

December 31, 2022