Nzioka waita

Aliyekuwa mgombea wa Ugavana katika kaunti ya Machakos kwenye uchaguzi mkuu wa Mwezi Agosti Nzioka Waita, ametangaza kuchukua mapumziko kutoka kwa shughuli za kisiasa kwa muda.

Akitoa tangazo hili kupitia mitandao yake ya Kijamii, waita ambaye alihudumu kama mkuu wa wafanyikazi katika ikulu ya Rais chini ya uongozi wa Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta, alisema kuwa amechukua uamuzi wa kujitenga na siasa ili kuangazia mkondo mpya wa Maisha yake na kujiendeleza kama mtu binafsi.

Mwanasiasa huyo ambaye aligombea ugavana wa Machakos kwa tikiti ya Chama Cha Uzalendo (CCU) alizoa jumla ya kura 129,181 dhidi ya Wavinya Ndeti wa chama cha Wiper ambaye ndiye gavana wa Sasa aliyezoa kura 226,609.

December 31, 2022