BY ISAYA BURUGU,18TH NOV 2022-Mbunge wa eneo bunge la Sirisia  John Waluke  ameachiliwa kwa dhaman aya shilingi milioni kumi pesa taslim na mahakama ya rufaa  kusubiri kusikilizwa kwa rufaa aliyowasilisha dhidi ya hukumu yake ya miaka 67.Haya yanajiri  baada ya Waluke mwezi jana  kuwasilisha rufaa dhidi ya hukumu hiyo aliyopewa na mahakama kuu  aikitaja kuwa kali muno na isiyohitajika.Hukumu ya mbunge huyo ilifuatia kesi ya ufisadi dhidi yake  ambapo anatuhumiwa kuilaghai bodi ya kitaifa ya nafaka na mazao NCPB  shilingi  milioni 313.Mbunge huyo alishatakiwa Pamoja na Grace Sarapay Wakhungu  na kampuni ya Erad Supplies & General Contracts Limited (Erad);  kampuni ambayo wawili  hao ni wana hisa.Waluke na Wakhungu, kupitia kwa kampuni hiyo walipaswa kusambaza mahindi tani alfu 40,00 kwa bodi ya  NCPB  mwaka  2004  lakini wakatia mfukoni  shilingi milioni 313  bila kusambaza mahindi hayo.

 

 

November 18, 2022