Rais William Ruto amezindua rasmi kiwanda cha kutengeneza chuma cha Devki katika eneo la kinango kaunti ya Kwale. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Ruto amesema kuwa serikali itaunga mkono kiwanda hicho ambacho kimegharimu shilingi bilioni 30 ili kutoa nafasi Zaidi za ajira kwa wakaazi wa eneo hilo.

Ruto vilevile ameeleza kuwa wakenya sasa wataweza kuagiza vifaa vya ujenzi humu nchini kupitia kiwanda hicho hatua ambayo itainua uchumi wa taifa.

Knado na hayo Ruto amedai kuwa  ukuaji wa viwanda nchini Kenya ulishuka katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kutokana na madai ya hujuma kutoka kwa watu wachache aliowataja kuwa walaghai na madalali.

Alisema, haya yalifanywa na watu hao ambao hawakutajwa majina wakishinikiza kubadilishwa kwa sera ya serikali ili kuongeza bidhaa kutoka nje na kupata punguzo tofauti na utengenezaji wa bidhaa za ndani, na hivyo kukatisha tamaa viwanda vya Kenya.

Kulingana na Ruto, mchango wa ukuaji wa viwanda katika Pato la Taifa (GDP) ulishuka kutoka 9% hadi 7%.

November 18, 2022