BY ISAYA BURUGU ,18TH NOV,2022-Waziri wa vyama vya ushirika Simon Chelugui ametoa mwelekeo kuhusu hazina ya hasla ambayo rais Wiliam Ruto anatarajiwa kuzindua mwishoni mwa mwezi huu.

Akizungumza na wandishi Habari afisini mwake,Waziri amesema kuwa masharti ya utoaji mikopo hiyo ambayo kiwango cha juu ni shilingi alfu 50,yatarahisishwa ili kila mkenya aweze kunufaika.Ili mmoja apate mkopo huo,serikali inapanga kutumia kampuni za huduma ya mawasiliano mabazo zitawezesha wakenya kuomba mikopo hiyo kupitia simu zao na pia kulipia mikopo yenyewe.

Hata hivyo hazina hiyo itakuwa na sehemu mbili ambapo sehemu ya kwanza ni mtu binafsi kuomba mkopo huo kupitia simu na sehemu ya pili itakuwa wafanyibiashara wanaolenga kuomba kiwango kikubwa cha pesaambao watahitajika kutuma ombi kwa benki na vyama vya mashirika vitavyochaguliwa kutoa mikopo hiyo.

Waziri vilevile amewaonya wananchi dhidi ya kulaghaiwa na watu wanaochapisha maelezo ya uongo mitandaoni kuhusu jinsi ya kuomba fedha hizo akisema hapatakuwa na ujumbe wowote kwenye mitandao kuhusu jinsi ya kuomba pesahizo.

 

 

November 18, 2022