BY ISAYA BURUGU 1ST FEB 2023-Shirika la reli nchini limetangaza kukumbatia mfumo wa kidijitali wa kulipia tikiti za usafiri katika usafiri wa treni za Madaraka Express.Agizo hilo la kupiga marufuku ulipaji wa pesa taslimu lilianza kutekelezwa Februari mosi ambapo wasafiri wote wameombwa kukumbatia mfumo wa kidijitali wa kununua tikiti kutumia M-Pesa.

Uhamiaji huu kutoka mifumo ya zamani hadi mifumo ya kisasa ya kidijitali ni moja ya ajenda kubwa katika serikali ya rais William Ruto, ambaye amekuwa akisema kwamba huduma nyingi katika ofisi za serikali zitakuwa zikitolewa kwa njia za kidijitali.

Hapo jana, rais aliongoza kikao cha baraza la mawaziri wake cha kwanza ambacho kilikuwa bila matumizi ya kalamu na karatasi, kwani waliohudhuria wote walionekana wakitumia vishkwambi na talakilishi.

Hiyo jana pia, serikali ilitangaza kwanzia mwezi Machi mwaka huu, vyeti vya kuzaliwa na vyqa kufa vyote vitakuwa vinatolewa kwa njia za kidijitali.

 

 

 

February 1, 2023