Muungano wa matabibu na madaktari wa meno nchini KMPDU umezitaka serikali za kaunti na ile ya kitaifa kuwaajiri matabibu zaidi waliohitimu katika masomo yao hivi karibuni.

Wakizungumza katika kikao na waandishi wa habari, Katibu mkuu wa KMPDU Dr. Davji Atellah amesema kuwa muungao huo umeshuhudia idadi ya juu ya matabibu waliohitimu wakiwa bila kazi huku hospitali nyingi nchini zikisalia na uhaba wa matabibu.

Naibu katibu wa KMPDU Dr. Miskellah Dennis amesema kuwa matabibu hao watasusia kazi iwapo hali itasalia hivi, akiwanyooshea kidole cha lawama maafisa wa serikali wanaogeuza gumzo na kuwakashifu matabibu kila wakati mkasa unapotokea hospitalini.

January 31, 2023