By Isaya Burugu,Oct 8,2022-Shirika la kulinda misitu nchini limetoa wito kwa wakulima kupanda miti mbali mbali kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.

Afisa msimamizi wa shirika hilo kaunti ya taita Taveta, Flavian Otieno anasema wanalenga kuwahamasisha wakulima kuhusu umuhimu wa upanzi wa miti hasa baada ya vyanzo vya maji kuanza kukauka.

Otieno vilevile ametoa wito kwa serikali ya kaunti na washika dau mbali mbali kushirikiana katika kupanda miti hiyo.

October 8, 2022