Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya kudhibiti Kawi na bei ya bidhaa za Petroli EPRA Daniel Kiptoo Bargoria ameagizwa kufika mahakamani Agosti 13 kwa kukiuka maagizo ya mahakama kuhusu Sheria ya Fedha ya 2023.

Mahakama Kuu ilitoa wito huo Jumatatu wakati wa kutajwa kwa ombi la Sheria ya Fedha.

Kiptoo aliagizwa kufika kortini ili kutoa sababu kwa nini hapaswi kuzuiliwa kwa kudharau maagizo ya mahakama yaliyotolewa na Jaji Mugure Thande kuhusu kusimamishwa kwa Sheria ya Fedha ya 2023.

Kesi ya dhidi ya Kiptoo iliwasilishwa na Seneta wa Busia Okiya Omtatah.

Itakumbukwa kwamba EPRA iliongeza VAT kwenye bidhaa za petroli kutoka 8% hadi 16% mnamo Juni 30, 2023 licha ya mahakama kusitisha kwa muda utekelezwaji huo.

Share the love
August 7, 2023