BY ISAYA BURUGU,09,NOV 2022-Maafisa wa polisi mjini Narok wamewatia mbaroni watu 18 wanaohusishwa na uuzaji wa pombe haramu mjini Narok.Kamishna wa kaunti ya Narok Isaac Masinde aliyedhibitisha kukamatwa kwao amesema kuwa oparesheni  hiyo ililenga wagemaji na watumizi wa pombe hiyo.

Vilevile amesema visa vya ugemaji na unywaji pombe hiyo haramu mjini Narok vinazidi kuongezeka kila kuchao na akawaonya wahusika kuwa watasakwa na kukamatwa.

Akizungumza na wandishi habari mjini Narok,Masinde pia amesema kikosi maalum kimebuniwa ili kufanya msako huo ambao ameongeza kuwa utaendelea hadi wahusika wote watakapotiwa mbaroni.

Uraibu wa matumizi ya pombe haramu mjini Narok umekuwa ukiongezeka kufuatia hattua ya vijana wengi kutokuwa na ajira.Mwanahabri wetu Antony Mintila ana ripoti hiyo kwa kina.

November 9, 2022