Rais William Ruto amekuwa mwenyeji wa rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ambaye yuko katika ziara rasmi ya siku mbili humu nchini. Akizungumza walipokuwa wakitoa taarifa ya pamoja katika ikulu ya rais jijini Nairobi, rais Ruto amepongeza hatua ya kuondolewa kwa masharati ya usafiri baina ya Kenya na Afrika kusini ambapo abiria wa kenya angepaswa kuwa na visa ili kusafiri nchini Afrika kusini. Rais Ramaphosa amesema kuwa safari hiyo itaanza tarehe mosi mwezi january mwaka 2023 na itakuwa ikifanyika kwa muda siku 90 kila mwaka.

November 9, 2022