Mshukiwa Mkuu wa Ujambazi North Rift akamatwa

Maafisa wa polisi katika kaunti ya Baringo wamefanikiwa kumtia nguvuni mshukiwa mkuu wa wizi wa mifugo na ujambazi katika maeneo ya Kaskazini mwa Bonde la Ufa. Mshukiwa huyo, Lonyangapat Amerinyang, alikamatwa mchana wa Alhamisi katika eneo la Kapedo Akoret, Kaunti Ndogo ya Tiaty.

Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi wa kaunti ya Baringo, Julius Kiragu, mshukiwa huyo amekuwa mstari wa mbele katika vitendo vya uhalifu, na amekuwa akiwindwa na maafisa wa polisi kwa muda wa miaka minne. Kukamatwa kwake kunachukuliwa kama hatua kubwa na muhimu katika kudhibiti na kuimarisha vita dhidi ya ujambazi katika ukanda wa kaskazini mwa Bonde la Ufa.

SOMA PIA: Wanasiasa 3 wahojiwa kuhusu ukosefu wa usalama Baringo na Samburu.

Polisi pia wamefanikiwa kupata bunduki mbili na risasi 15 ambazo mshukiwa huyo alikuwa akizimiliki, na kufikisha idadi ya bunduki zilizopatikana hadi sasa kuwa tatu. Kamishna wa kaunti ya Baringo Stephen Kutwa kwa upande wake amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na polisi kukabiliana na ujambazi, akieleza kwamba taarifa za wananchi zimewasaidia pakubwa katika vita dhidi ya ujambazi. 

Kukamatwa kwa Lonyangapat kumeifikisha idadi jumla ya majambazi ambao wamekamatwa hadi watatu, katika huku bunduki tatu kwa jumla zipatikana hadi sasa.

Share the love
November 16, 2023