Kinara wa Azimio la umoja Raila Odinga ameitaka serikali kuweka wazi mkataba wa ununuzi wa mafuta uliotiwa saini kati ya Kenya, Saudi Arabia na UAE akitaja ulaghai na ufisadi kwenye mkataba huo.

Kwenye kikao na waandishi wa habari, Odinga amesema kuwa mkataba huo ndio chanzo cha kupanda kwa bei ya mafuta nchini. Ameongeza kuwa Kenya haikutia saini mkataba wowote na UAE au Saudi Arabia na kwamba mkataba huo ulitiwa saini kati ya Wizara ya kawi na kampuni zinazomilikiwa na serikali katika eneo la Mashariki ya Kati.

Share the love
November 16, 2023