Jaji mkuu Martha Koome amemapisha rasmi Amin Ibrahim Mohammed kama mkrugenzi mpya wa idara ya jinai katika jengo la mahakama ya juu jijini Nairobi asubuhi ya leo.Ibrahim anachukua nafasi ya George Kinoti aliyejiuzulu mwezi jana.

Akizungumza baada ya kuapishwa,Ibarahim ameapa kuwatumikia wakenya kwa uadilifu na weledi kwa kuzingatia katiba ya kenya.Aidha Ibarhim amewaacha wengi kinywa wazi baada ya kuweka wazi nambari yake ya simu kwa umma ili yeyote anayetaka kuzungumza naye anaweza kumfikia kwa urahisi.

October 19, 2022