BY  ISAYA BURUGU,10,NOV 2022-Mtu mmoja ameaga dunia baada ya kupigwa na umma akifumaniwa kuiba Ng,ombe eneo la Trasmara kusini.

Akithibitisha kisa hicho naibu kamishana wa Trasmara kusini George Onyango amesema Jamaa huyo ameuawa katika kaunti jirani ya Migori eneo la Kehanja  katika soko la Ng,ombe baada yake kujaribu kutoroka akiwa na Ngo,mbe ambao waliibwa kutoka eneo Trasmara kusini.

Onyango amesema Jamaa huyo alipeleka mifugo aliyoiba katika soko la Kehanja hatua ambayo imepelekea kukamatwa kwake na mwenye Ng,ombe hao .

Onyango amesema mafisa wa upelelezi wa jinai DCI wanaendelea kuchunguza  kisa hicho.Onyango wakati huo huo amewataka wananchi wasichukue sheria mikononi mwao

November 10, 2022