Gideon Moi

Kinara wa Chama cha Kanu Gideon Moi amejiondoa katika kinyang’anyiro cha kuwania wadhifa wa kuliwakilisha taifa katika bunge la Afrika Mashariki (EALA)

Kwa mujibu wa Taarifa ya Katibu wa maswala ya kisiasa katika chama cha KANU Fredrick Okango seneta huyo wa zamani wa Baringo amechukua hatua ya kujiondoa katika mbio hizo ili kutoa nafasi yake kwa viongozi wengine. Moi ambaye ni mmoja wa vinara waliounda muungano wa Azimio la Umoja, alipendekezwa kama mmoja wa viongozi watakaowakilisha taifa katika bunge hilo, huku muungano tawala pia ukitoa orodha ya viongozi 15 kuwania nyadhifa 9 za uwakilishi.

Katika Mpango wa kuwatuma wawakilishi wa taifa la Kenya kwenye bunge hilo, muungano wa Kenya Kwanza umetengewa nafasi 5 za uwakilishi kati ya kati ya 9, huku Muungano wa Azimio la Umoja One Kenya Alliance ukipata nafasi nne.

November 9, 2022