Naibu wa Rais Rigathi Gachagua ameahidi kuwa wakenya hawatakua na haja ya kuhofu kuhusu kufurushwa makwao kiholela au kubomolewa makaazi yao nyakati za usiku.
Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa shule ya Komarok jijini Nairobi alikoandamana na Rais William Ruto, Gachagua amesema kwamba serikali ya Rais William Ruto imetoa ilani kwa viongozi wote watakaotekeleza maagizo yoyote ya kuwafurusha wananchi kutoka kwa makaazi yao pasi na kujadiliana na idara za usalama katika kaunti husika. Naibu wa rais amesisitiza wakenya watakao furushwa kutoka katika ardhi ambayo si yao watapata maeneo mbadala watakapoishi.
SAUTI: Kauli ya Naibu wa Rais Rigathi Gachagua
Katika hafla hiyo aidha, Rais William Ruto aliahidi kuwa wizara ya ardhi imeanzisha juhudi za kutoa zaidi ya hatimiliki 4000 za shamba kwa wakaazi katika kaunti ya Nairobi, kama mojawapo ya njia za kukabiliana na matatizo yanayoibuka kuhusu ardhi katika kaunti hiyo pamoja na kutoa nafasi kwa wananchi kutekeleza miradi ya maendeleo bila hofu.
Soma Pia
- Serikali ya Narok Kugharamia Ada za Mazishi kufuatia Mauaji ya Angata Barrikoi. April 29, 2025
- Ibada ya misa ya wafu yaandaliwa kumuaga Papa Francis. April 25, 2025
- Kadinali Kevin Farrell, kuongoza Ibada ya Kufunga Jeneza la Hayati Papa Francis. April 24, 2025
- Mwili wa Papa Francis wahamishwa hadi Kanisa Kuu la St. Peter’s Basilica mjini Vatican. April 23, 2025
- Mwili wa Papa Francisko Wawasili katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro April 23, 2025