Tume ya Utumishi wa Umma (PSC) imetoa mwaliko kwa wananchi wenye nia ya kuwania nafasi ya makatibu waratibu katika wizara mbalimbali (CAS) kutuma maombi yao ya nafasi hizi kabla ya Oktoba 27. Katika taarifa iliyochapishwa Jumatano 12.10.2022 na mwenyekiti wa PSC Anthony Muchiri, wanawake, watu kutokaa jamii za walio wachache pamoja na walemavu wamehimizwa kuchuua nafasi hii kutuma maombi yao ya kazi hizi.

Baadhi ya matakwa kutoka kwa wananchi wanaopania kutwaa kazi hizi ni pamoja na Shahada kutoka chuo kikuu kinachotambuliwa nchini Kenya, pamoja na uwezo wa kutoa uongozi katika nafasi za umma ikiwemo kuzingatia kifungu cha sita cha katiba kuhusu maadili ya viongozi katika nyadhifa za umma.  Mengine yanayohitajika ni pamoja vyeti kutoka kwa Mamlaka ya ukusanyaji Ushuru nchini (KRA), Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HELB) na Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC).

October 12, 2022