BY  ISAYA BURUGU 21ST DEC 2022-Kila mwanafunzi aliyefanya mtihani wa kitaifa kwa darasa la nane mwaka huu atapata nafasi katika shule ya upili.Waziri wa elimu Ezekiel Machogu anasema serikali maho kuendelea na mpango wake wa Watoto kujiunga na shule kwa asilimia mia kwamia.

Watainiwa 2, 531, 785  kote nchini   waliofanya mtihani huo   ambapo , 1,244, 188  kati  yao  walikuwa watainiwa wa KCPE   1, 287,597 wakiwa wa gredi ya sita watapata fursa kujiunga na shule za upili Matokeo ya mwaka huu yalimarika ikilinganishwa nay a mwaka jana ambapo mwanafuzni bora alisajili alama 431 ikilinganishwa na alama  428 zilizosajiliwa na mwanafuzni  bora katika mtihani wa mwaka jana.

. Kaunti zilizokuwa na kiwango cha juu cha watainiwa  waliokuwa chini ya umri wa miaka 12  zilikuwa ni Baringo,Kericho,Bomet,Wajir na pokot Mgharibi.Kunti zilizokuwa na idadi ya juu ya watainiwa waliohitimu miaka  18 ni Garisa,Kwale,Turkana, Kilifi na Mandera.Watainiwa wanaweza kupokea matokeo yao kwa kutuma ujumbe mfupi ulio na nambari yao ya usajili yaani index number kwa nambari ya  ujumbe mfupi 20076

 Wakati huo huo Zaidi ya watainiwa milioni 1.2 wa gredi ya sita  waliofanya mtihani wa  kwanza chini ya mtaala mpya wa CBC KAPSEA  watapokea ripoti zao kufikia tarehe 16 mwezi Januari mwakani.Katika mtihani wa mwaka huu watainiwa walirekodi matokeo bora katika karatasi nne ikilinganishwa na mwaka jana.Kwa mjibu wa Waziri Machogu ni kwamba mtihani wa Kingereza  lugha,Kiswahili Luga,Kiswahili nsha na mtihani wa lugha ya ishara watainiwa walirekodi matokeo bora.Hata hivyo katika karatasi zingine sita matokeo hayakuwa yakuridhisha sana. Nazo ni kuandika Kingereza ,Kuandika lugha ya ishara,sayansi,somo la kijamii na hesabati.Aidha watainiwa wakike walifanya vyema kuliko wenzao wakiume katika somo la kingereza,Kiswahili na lugha ya ishara,huku wenzao wakiume wakisajili matokeo bora kwenye masomo ya hesabati,sayansi,somo la kidini na somo la kijamii.

.Kwa ujumla makundi mbali mbali ya watainiwa hao wakiwemo wale wenye mahitaji maalum walisajili matokeo yaliyoimarika.

December 21, 2022