BY ISAYA BURUGU 21ST DEC 2022-Mwanamume mmoja mwenye umri wa makamo kutoka eneo la Magena, kaunti ya Kisii anapigania macho yake baada ya umati wa watu kumvamia katika shambulizi linaloshukiwa kuwa mzozo wa kimapenzi.

Polisi, hata hivyo, walisema Simon Kengere mwenye umri wa miaka 40, alipatikana akirandaranda kwa nia mwendo wa saa nane usiku wa kuamkia Jumanne na kwamba alikimbizwa hospitalini huku akivuja damu machoni.

Hata hivyo, alifafanua kuwa kulikuwa na tetesi nyingi kuhusu tukio hilo na kuongeza kuwa wanaendelea kufanya uchunguzi.

Alisema hata hivyo bado wanaangalia taarifa hizo zote huku wakitafuta kutofautisha ukweli na propaganda.Opondo alisema Kengere alikimbizwa katika Hospitali ya Gucha, eneo la Ogembo kwa matibabu ya dharura lakini kufikia Jana jioni familia ilikuwa inatafuta rufaa ili apelekwe katika kituo tofauti cha afya kwa matibabu ya hali ya juu.

Akiwa Gucha, Kengere alisema alitobolewa macho na watu waliompata kwenye nyumba ya mchumba wake.

 

 

 

December 21, 2022