BY ISAYA BURUGU,22ND FEB,2023-Mungano wa Azimio la umoja umeandaa  maombi yakitaifa katika bustani ya Jevanjee jijini Nairobi.Kwa mjibu wa viongozi wa mungano huo, maombi hayo yanalenga kumsihi muungu kuinglia kati  masaibu yanayowakumba wakenya yakiwemo gharama ya juu ya kimaisha na kiangazi.Hafla hiyo imeanza kwa maombi kutoka kwa viongozi wadini mbali mbali.

Katika hafla hiyo viongozi waserikali wametakiwa kujitahidi kufanyia wananchi kazi kando na kuandaa maombi. Vilevile serikali imetakiwa kurudisha ruzuku kwa uchumi wa nchi ili kuwapunguzia wannachi mzigo mzito wakimaisha.

Kinara wa Azimio la umoja Raila Odinga akisema kuwa ni sharti hilo lifanyike la sivyo wataishurutisha serikali kutekeleza hilo.Hafla hiyo inakuja wakati ambapo rais Wiliam Ruto amekuwa akiongoza hafla mbali mbali za maombi sawia.

Tayari hafla kama hizo zimeandaliwa katika kaunti hii ya Narok,Nakuru a wa hivi punde Zaidi ukiwa katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.Yote ambayo imehudhuriwa na rais Ruto.

Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Azimio wakiwemo,Kinara Raila Odinga,kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka Martha Karua wa Narc Kenya,seneta wa Narok Ledama Ole Kina kati ya wengine.

 

February 22, 2023