Mvua inayotarajiwa kunyesha kati ya mwezi Machi na May mwaka huu haitafikia kiwango kinachohitajika ili kuokoa athari za kiangazi zinazoendelea kushuhudiwa humu nchini.

Wanasayansi na watabiri wa hali ya hewa wameeleza kuwa mvua hiyo inatarajiwa kuwa chini ya milimita 400.

Kwenye kikao kuhusu mazingira, waziri wa mazingira Soipan Tuya amedokeza kuwa kuna haja ya kuimarishwa kwa huduma za kutabiri hali ya anga humu nchini.

Wakati hayo yakijiri kongamano la 21 la mazingira barani Afrika limengoa nanga jijini Abdjan nchini Cordivoire ambapo washiriki wanatarajiwa kubadili mawazo ili kusaka suluhu kwa mabadiliko ya hali ya hewa na uchafuzi wa mazingira.

Kongamano hilo linahudhuriwa na watalamu  kutoka nchi mbali mbali Afrika. Kenya pia inawakilishwa na wawakilishi  kutoka mashirika mbali mbali yanayojihusisha na utunzaji mazingira humu nchini.

Itakumbukwa kwamba kongamano hilo linandaliwa wakati uchafuzi wa mazingira unazidi kushuhudiwa haswa kutokana na uchafuzi wa mitaa ya mabanda.

 

February 22, 2023