BY ISAYA BURUGU,20TH FEB,2023-Wezi wa mifugo eneo la Olmelil Trasmara magharibi wameonywa kuwa chuma chao kimotoni.Akiwahutubia wenyeji wa Olmelil katika mipaka ya kaunti ya Narok na kaunti ya Nyamira chifu wa eneo la Kapune Emmanuel Nakuso amesema serikali haitawasaza wanaojihusisha na wizi wa mifugo na kwamba watachuliwa hatua kali za kisheria.

Chifu huyo  amesema licha ya serikali kuendesha oparesheni katika eneo hilo bado kuna wa wezi waliopatiikana  wakiimba mifugo na kufuruga amani kati ya  jamii mbili zinazoishi eneo hilo.Nakuso amesema vikosi vya usalama viko  macho kukabiliana na wanaovunja sheria ya taifa hili.

Wakati huo huo chifu huyo amesema oparesheni ya kunasa pombe haramu pia inaendelea eneo hilo hii ni baada ya wengi wa wakaazi wa eneo hilo kukumbatia uraibu wa unywaji pombe haramu ya  changaa ,kangara na busaa.

Ni hulka  ambayo inaripotiwa kuwadhiri  wanafunzi wengi huku wakiacha  masomo yao kutokana na umaskini baada ya wazazi wao kuigilia uraibu wa unywaji pombe kipindukia.

February 20, 2023