Mwanafunzi mmoja anaendelea kufanyia mtihani wake wa KCSE katika hospitali ya Ololulunga Narok kusini baada ya kujifungua.

Kwa mujibu wa naibu kamishana wa Narok kusini Felix Kisalu,mwanafunzi huyo amejifungua mtoto wa kike na yuko katika hali nzuri. Aidha Kisalu ameeleza kuwa mwanafunzi huyo ametengwa katika chumba maalum ambako anafanya mtihani wake bila tashwishi yoyote.

Hali kadhalika Kisalu amesema kuwa kamati ya usalama imezuru eneo hilo nzima kutathmini hali ya watahiniwa wanaoandika mitihani hiyo ya kitaifa.

December 7, 2022