BY ISAYA BURUGU 7TH DEC 2022-Watoto wanne wamelazwa hospitalini wakiwa hali mahututi  baada kudaiwa kupewa sumu  na kudungwa kisu na baba yao  kabla yake kuaga dunia kufuatia kujitia kitanzi.

Kisa hicho kinaripotiwa kutekelezwa kwenye  yao ya kukodi  katika kituo cha  kibiashara cha Nyagoro lokesheni ya Kochia mashariki kaunti ya Homa Bay.

Watoto  hao wa kati ya miaka mitatu na tisa walijeruhiwa vibaya na baba yao aliyetambuliwa kama Ronnie Ochieng’ Nyore  usiku wa kuamkia leo  kufuatia madai ya mzozo wa kinyumbani kati yake na mkewe.Kwa mjibu wa chifu wa lokesheni ya Kochia Mashariki Kennedy Odero aliyefika eneo la tukio,Ronnie  aliwadunga kisu tumboni Watoto hao kitumia  kisu cha nyumbani   baada kudaiwa kuwapa sumu  ya  kuua wadudu.

December 7, 2022