BY ISAYA BURUGU,23RD FEB,2023-Maafisa wa polisi kaunti ya Homa Bay wanamzuilia mwanamke wa miaka 23 anayetuhumiwa kumu ana kutupa mwili wa mtoto wake mchanga baada ya kumzaa nyumbani mwake katika mtaa wa Makongeni mjini Homa Bay.
Mwanamke huyo alikamatwa baada ya wakaazi wa Makongeni kuupata mwili wa mtoto huyo kakatika jaa la kutupa taka.
Kwa mjibu wa naibu chifu wa lokesheni ndogo ya Simenya Erick Odhiambo, mshukiwa alikamatwa na polisi baada ya kundi la wanawake na afisi yake kuendesha msako wa mwanamke yeyote ambaye amezaa na kumtupa mwanawe ndipo walipompata mwanamke huyo.
Amesema mshukiwa aliwadhibitishia polisi kuwa yeye ndiye aliyekuwa amemua na kutupa mwili wa mtoto huyo hata ingawa hakutoa sababu za kitendo hicho.
Kamanda wa polisi kaunti ya Homa-Bay Samson Ole Kinne amedhibitisha kukamatwa kwa mwanamke huyo ambaye anazuiliwa akisubiri kufikishwa mahakamani.