BY ISAYA BURUGU 23RD FEB,2023-Waziri wa Elimu katika serikali ya kaunti ya Narok Rotich Simotwo ametoa wito wakukomesha kabisa maswala ya ukeketaji na ndoa za mapema kaunti ya Narok.

kwenye mahojiano ya kipekee na wandishi wa habari wakituo hiki ofisini mwake,Simotwo amesema japo visa hivyo vimepungua kwa asilimia ndogo wakati huu ukilinganisha na miaka ya hapo awali kuna haja ya kuongeza jitihada za kutokomesha kabisa visa hivyo.

Kwa mjibu wa Waziri huyo visa vya mimba za mapema na ukeketaji  vimepelekea  kaunti ya Narok kusalia nyuma  haswa kwenye elimu .

 

Wakati uo huo Simotwo amewashukuru washikadau mbali mbali wa elimu kwa kukaza kamba kufanikisha vita dhidi ya ukeketaji mimba na ndoa za mapema visa ambavyo amesema vimekuwa kizingiti kikuu kwa mtoto wa kike kupata elimu.

 

 

 

 

 

February 23, 2023