BY ISAYA BURUGU,12TH SEPT,2023-Msusi aliyetoweka wiki mbili zilizopita amekutwa ameuawa na mwili wake kutupwa kwenye shimo la choo eneo la Mlolongo, kilomita chache kutoka kwenye kituo chake cha kazi.Taarifa zasema kuwa  Mwili huo uliokuwa ukioza wa Jane Mwende Mwanzia mwenye umri wa miaka 29 uligunduliwa baada ya washukiwa kuwaongoza polisi kwenye eneo la tukio.Washukiwa hao ambao walikamatwa wiki jana kuhusiana na kutoweka kwa Mwende awali walikuwa wamewahadaa maafisa wa upelelezi katika msitu wa Magongo eneo la Wote kaunti ya Makueni.

Katika hali ya kushangaza, washukiwa hao baadaye walibadilisha maelezo yaliyowaongoza polisi hadi  Kiserian kabla ya kufichua eneo halisi ambapo mwili wa Mwende uligunduliwa huko Mlolongo.

Familia, marafiki na wafanyakazi wenzake wa Mwende wamekuwa kwenye harakati za kumtafuta alipotoweka wiki mbili zilizopita—wameenda katika vituo vingi vya polisi, hospitali na hata kwenye vyumba vya kuhifadhia maiti bila mafanikio.Jane Mwende anasemekana kupokea simu mapema asubuhi ya Ijumaa, Agosti 25 kutoka kwa mtu aliyejifanya mteja aliyehitaji huduma zake za unyoaji nyumbani kwao.

Aliondoka asirudi tena. Wasiwasi ulizidi pale Jane aliposhindwa kuripoti kazini siku iliyofuata. Simu yake ilibaki imezimwa.Kutoweka kwa Jane kulionekana wazi alipokosa kumchukua mtoto wake kutoka nyumbani kwake Yatta huko Machakos baada ya likizo ya Agosti.

 

 

 

 

 

 

 

September 12, 2023