Wanabodaboda chini ya muungano wa Eminent jijini Nairobi, hii leo wamefanya mkutano na wakuu wa polisi kutoka eneo hilo kufuatia ongezeko la visa vya uhalifu vinavyodaiwa kutekelezwa na waendesha bodaboda.

Akizungumza wakati wa mkutano huo, kamanda wa oparesheni katika kituo cha polisi cha Central David Apima, amewahimiza wanabodaboda kujiunga na vyama vya ushirika ili waweze kusajiliwa na kutambulika kama wanabodaboda halali.

Hali kadhalika amewataka wanabodaboda hao kushirikiana na maafisa wa usalama kwa kuwashtaki wenzao wnaokaidi sheria za uendeshaji bodaboda.

November 12, 2022