BY ISAYA BURUGU,4TH FEB,2023-Mwili wa mwanamme aliyezama katika mto Nyamindi katika Kijiji cha Ngucui katika kaunti ya Kirinyaga  umoendolewa  majini.Mwili huo uliondolewa  na wapiga bizi wa kibinafsi na wenyeji waliojitolea.

Kelvin Muthomi  ambaye  ni mfanyikazi wa  hoteli  moja mjini Kimbimbi  eneo bunge la Mwea  alikuwa amekwenda  katika mto huo  kusherehekea siku yake ya kuzaliwa akiwa na mpenziwe  na rafiki alipoteleza na kuanguka majini.

Akizungumza baada ya  mwili wa Muthomi kuondolewa majini ,babake marehemu Duncum Mutuma anayetoka kaunti ya Meru amesema alipigwa  na mshangao  baada ya kupokea  ujumbe wa kifo cha mwanawe na akajikaza na kufika eneo la mkasa.

Mutuma ambaye alikuwa ameandamana na  jamaa wa familia yake na marafiki anasema ,wapiga bizi walishinda mchana kutwa  wakitafuta mwili wa mwanawe  hadi mwendo wa saa moja unusu jioni walipofanikiwa kuupata.

Mwili huo umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Kibugi mjini Kimbimbi ukisubiri upasuaji.

 

 

February 4, 2023