Serikali inapania kuagiza mbolea kutoka nchini Tanzania kuanzia julai mwaka huu.Taasisi ya utafiti wa kilimo na mifugo KALRO imepatiwa jukumu la kukagua ubora wa mbolea hiyo.

Kwa mujibu wa waziri wa kilimo Mithika Linturi ni kwamba hatua hiyo inapania kuwasilisha mbolea ya bei nafuu kwa wakulima ili kuongeza uzalishaji wa chakula humu nchini.

Linturi ameeleza kuwa mbolea ya FOMI  asilimia 50 ni halisi na asilimia 50 iliyosalia ni kemikali  hivyo kupunguza gharama. Hali kadhalika ameongeza Serikali ina lengo la  kuongeza uzalishaji wa bidhaa za kilimo kwa kupunguza gharama ya mbolea.

February 4, 2023