Walimu saba waliokamatwa kwa kosa la kuwadhalilisha wanafunzi wa gredi ya pili wa shule ya Itumbe D.O.K watazuiliwa kwa siku mbili zaidi katika kituo cha polisi cha Inguso.

Hakimu wa mahakama ya Ogembo Paul Biwott amesema amewapa maafisa wa upelelezi siku hizo mbili kukamilisha uchunguzi wao.

Aidha upande wa mashtaka ulitaka kuwazuilia kwa saba zaidi.

Katika barua sita tofauti zilizoandikwa na mkurugenzi wa TSC wa Kaunti Ndogo ya Nyamache James Wanyela, walimu James Oigoro Ocharo, Wilfred Momanyi Ochenge, Florence Nyabuto, Isaac Osoro, Morara George Igworo na Odong’a Obedi Nyanchong’i wamehamishwa hadi shule ya msingi ya D.O.K. hii leo ili kuchukua nafasi ya walimu waliosimamishwa kazi na TSC.

Walimu waliosimamishwa kazi ni pamoja na Everlyne Moraa, Angelina Joseph, Catherine Mokaya, Moraa Nyairo, William Isuka na Gladys Kenyanya kwa kukiuka vifungu vya 9 (1) na (c) (11) vya Jedwali la Tatu la Sheria ya TSC, 2012.

February 3, 2023