Naibu Spika wa Bunge la Kitaifa na ambaye pia ni  Mwakilishi wa kina mama kaunti ya Uasin Gishu Gladys Boss Shollei ameunga mkono sheria za ushuru ambazo zimpendekezwa na serikali akisema zitasaidia kuwaondoa Wakenya katika hali mbaya ya kiuchumi.

Akiyatetea mapendekezo yaliyotolewa katika Mswada wa Fedha wa 2023 ambayo yameibua mizozo kati ya viongozi,Shollei amedokeza kuwa mswada huo umejikita katika kuinua maisha ya wakenya wa kipato cha chini kutoka kwa mzigo wa ushuru uliopo.

Aidha amedai kuwa Wakenya wanadanganywa na wale wanaopinga mswada huo na badala yake amewataka kuchukua muda kuchunguza mapendekezo hayo kwa kina.

Share the love
June 5, 2023