Gavana wa kaunti ya Narok Patric Ntutu aliwaongoza viongozi wengine wa serikali ya Kauti katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika Wadi ya Keekonyokie eneobunge la Narok Mashariki.

Gavana Ntutu aliyekagua ujenzi unaoendelea wa bwawa la Duka Moja, aliutaja mradi huu kama moja ya miradi muhimu katika kutatua tatizo la uhaba wa maji kwa wananchi katika eneo hilo. Aidha alisisitiza kujitolea kwa serikali yake katika utekelezaji wa miradi ya maji, katika awamu ya kwanza na ya pili ya miradi ya CIDP.

Gavana Ntutu pia katika ziara yake hii leo, alizindua vibanda vya wachuuzi wa mahindi katika eneo la Junction, vitakavyowasaidia kuendeleza biashara zao bila mahangaiko hasa nyakati za mvua.

June 3, 2023