Muungano wa viongozi wa kidini nchini NCCK, umetoa wito wa kuhusishwa kwa wananchi kabla ya serikali kufanya maamuzi muhimu yanayoathiri wananchi wake.

Katika taarifa yao alasiri ya leo, viongozi hao wamerejelea hatua ya kuondolewa kwa marufuku dhidi ya vyakula vya Kisaki almaarufu GMO wakiitaka serikali kuwahusisha wananchi kabla ya kutoa uamuzi wa kuiondoa marufuku hiyo.

Viongozi hao aidha wamesifia hatua ya serikali kuwapa ulinzi wa kutosha viongozi wa upinzani wakati wa mkutano wao hio jana, wakisema kuwa hii ni ishara ya kuimarika kwa demokrasia humu nchini, wakisema kuwa uhuru huu utaimarisha utangamano wa wakenya kutoka maeneo yote ya taifa.

December 8, 2022