Baraza la kitaifa la makanisha humu nchini NCCK limeorodheshwa kama mojawapo ya mashirika mbalimbali yaliyoteuliwa ili kutwaa tuzo la Kimataifa la Nobel Peace Prize, kufuatia mchango wake katika kuhamasisha amani wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

Baraza hilo lilikuwa baadhi ya mashirika yaliyoandaa vikao vya aina mbalimbali kabla na hata baada ya uchaguzi, kuwahimiza wakenya kuendelea kushirikiana na kuishi Pamoja kama ndugu.

Katika taarifa yao kufuatia uteuzi huo, viongozi wa baraza hilo wameeleza furaha yao, wakitaja uteuzi huo kuwa wa muhimu Zaidi, sio tu kwa ajili ya kazi walizofanya hapo awali, bali hata kwa kuwapa moyo wa kuendeleza kazi hii siku za usoni.

https://twitter.com/NCCKKenya/status/1626878539927519233?s=20

February 18, 2023