Hazina ya Kitaifa ya Bima ya Afya (NHIF) imetupilia mbali uvumi unaodai kuwa hazina hiyo imesitisha mpango wa Linda Mama kutoka kwenye orodha huduma zake.

Rais mstaafu Uhuru Kenyatta alianzisha mpango huo wakati wa utawala wake katika jitihada za kuboresha upatikanaji wa huduma bora za afya ya uzazi, na kuimarisha viwango vya matibabu ya watoto wachanga ili kuifikia ruwaza ya Kenya ya mwaka 2030 pamoja na Ajenda ya Maendeleo Endelevu.

Katika taarifa yake kwa umma, NHIF imesisitiza kuwa mpango huo ungali unaendelea na umewafaidi wanawake milioni 6 tangu kuanzishwa kwake. NHIF pia imewataka wakenya kutahadhari na kuwa makini kuhusu jumbe zinazoenezwa kwenye mitandao ya kijamii.

January 3, 2023