galana-project-bg

Rais William Ruto amebatilisha uamuzi wake kuhusu mpango wa kugawanya mradi wa ukulima wa unyunyizaji wa Galana Kulalu.

Katika chapisho alasiri ya Leo, Rais Ruto amesema kuwa mradi huo badala yake utatumiwa katika uzalishaji wa mahindi katika arthi ya ekari 10,000 iliyo tayari kuanzia mwezi ujao, chini ya mpango wa ushirikiano kati ya serikali ya kitaifa na mashirika ya kibinafsi, mpango utakaoendelea kwa kipindi cha miezi 6 ijayo.

Mradi wa Galana Kulalu uliigharimu serikali takriban dola bilioni 5 ili kusaidia taifa kukabiliana na tatizo la ukosefu wa chakula.

January 3, 2023