Nick Salat

Chama cha KANU kimemsimamisha kazi Katibu Mkuu wa chama hicho Nick Salat kwa madai ya utovu wa nidhamu na ukiukaji wa katiba ya chama.

Kwa mujibu wa barua ya Mwenyekiti wa Kitaifa wa KANU Gideon Moi kwa Halmashauri Kuu ya Kitaifa ya chama hicho (NEC), Bw Salat amesimamishwa kazi mara moja akisubiri kupigwa msasa na kamati ya nidhamu ya chama hicho inayotarajiwa kutoa mapendekezo yake katika kipindi cha siku 30 zijazo.

Salat kwa upande wake hata hivyo amepinga vikali uamuzi huo, akisema kuwa Gideon Moi hana uwezo wowote wa kumsimamisha kazi,a kiongza kuwa wote wawili wanashikilia nyadhifa zao kikaimu.

December 15, 2022