Hukumu ya maafisa watatu wa polisi na raia mmoja waliopatikana na hatia ya mauaji ya Wakili Willie Kimani, mteja wake Josephat Mwenda na dereva wa teksi Joseph Muiruri itatolewa tarehe 3 mwezi februari mwaka ujao.

Wanne hao ni pamoja na maafisa Fredrick ole Leliman, Stephen Cheburet Morogo, Sylvia Wanjohi na mtaarifu wao Peter Ngugi.

Wakili Kimani na wenzake wawili waliuwawa miaka sita iliyopita ambapo walitekwa nyara kutoka kwa gari lao walipokuwa wakitoka katika mahakama ya Mavoko.

Kulingana na polisi, baada ya kutekwa nyara, watatu hao walizuiliwa kwa saa chache katika kituo cha polisi cha Syokimau kabla ya kupelekwa kwenye uwanja ambapo waliuawa. Miili yao ilipatikana imetupwa kwenye Mto Oldonyo Sabuk ikiwa imefungwa kwenye mifuko nyeusi.

December 16, 2022