Baraza la madhehebu mbalimbali nchini limewapongeza wakenya na haswa vijana kwa kudumisha amani wakati na baada ya uchaguzi mkuu.

Kwenye kikao na waandishi wa habari, viongozi wa baraza hilo wamesema kuwa vijana walikubali wito kutoka kwa viongozi wa kidini na mashirika ya amani kuzingatia utangamano na kutokubali kutumika vibaya na wanasiasa.

Kuhusiana na suala la kubuniwa kwa afisi ya upinzani, viongozi hao wamemtaka rais William Ruto kuandaa kikao cha wananchi ili waweze kutoa maoni yao kuhusu pendekezo hilo kabla ya katiba kufanyiwa mageuzi.

December 15, 2022